Kwakweli selikali yetu sijui hata inaelekea wapi jamani mana kutokana na mauaji yalio tokea week hii huko Tegeta yanasikitisha sana kwa kugombea mambo ya viwanja.sikufatilia kiundani hili swala tangu wananchi wa tegeta walipo ambiwa wajiandae kuhama na kwamba nyumba zao zitavunjwa.ila hii sura mpya iliojitokeza wananchi kupigana mapanga na kuuana imesikitisha kwa kweli,kuna watu inadaina wametumwa na kampuni kuja kuvunjia wananchi wa tegeta nyumba zao na ruksa walipewa na selikali,mwishowe wananchi nao hawakukubaliana na swala hilo na walipokusanyika na kuanza kuwapiga hao watu waliotumwa kuja vunja nyumba zao.
WATU WALIVYO CHINJANA
je inakuwaje kampuni binafsi inatumwa kwenda kuvamia wananchi ,kama ni hivyo selikali ilishindwa ata kuagiza polisi wawepo kwenye zoezi hilo.
swali linakuja selikali wapo wapi siku zote kupima maeneo yote kabla watu hawajaanza ujenzi,na watu wakajua hapa itapita barabara ,na maelezo mengine ila hao swala hili hulikwepa na kusubiria kuona raia washajenga ndio wao wapeleke matumbo yao kupanga kubomoa,Jamani swala la kujenga ni gumu mtu kumudu kununua kiwanja inamgharimu mda sasa swala la kujenga nyumba si ni miaka na miaka ila selikali haijali hilo inamoboa nyumba ya mtu kwa dakika wakati katumia miaka kuijenga kweli ni haki hii. kwa upande mwingine naungana na wananchi kwa kutetea mali zao ingawa hawaja watendea haki wale marehemu adhabu walio wapa ni kubwa mno.na wamewapa pengo kubwa familia zao.hope selikali itajifunza kupitia hili ,kheri ya mwizi ataiba Tv na kukuachia nyumba yako kuliko anaeivunja na kukufanya kama mkimbizi ndani ya nchi yako.
No comments:
Post a Comment