Sep 10, 2011

WATANZANIA WAFA MAJINI ZANZIBAR

Ajali ya meli mbaya imetokea zanzibar usiku wa jana kuamkia leo ya meli itwayo spice islander iliyokuwa imetokea Bandari ya malindi Unguja na kuelekea Pemba ,ilikuwa imebeba abiria 610 na mizogo ambayo hawakusema ilikuwa na uzito gani.

ingawa walibahatika kuwaokoa watu 250 na wengine bado wapo majini ,mungu awabariki watoke salama na waliofariki mungu awalaze pema peponi,ni pigo kubwa kwa watanzania wenzetu walio poteza ndugu na jamaa.watanzania tubadilike jamani mbona tamaa mbele ya pesa inatuletea madhara makubwa kama haya inasemekana meli ilijazwa watu wengi na migizo tofauti na idadi inayotakiwa sasa swala kama hili ni dogo kulitatua sema tamaa imeeleta madhara.

2 comments:

Anonymous said...

Jamani hili ni tukio la pili kubwa la ajali ya vyombo vya majini, watanzania bado madonda ya m.v Bukoba tunayo, na uzembe ni huo huo wa kujaza mizigo na watu, hivi vyombo havikaguliwi kabla ya kuanza safari? jamani inabidi mamlaka zinazohusika kuanzia waziri mwenye dhamana mpaka mfunga na mfungua nanga wajiuzulu nyadhifa zao na wahukumiwe kwa uzembe.

mama wa kitanzania

Anonymous said...

mungu awatangulie viongozi hawajui kazi zao na haina haja ya kuwaita viongozi mana wanalijua ila wanalifungia macho pumbavvvvvvvvvvvvvv zao

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...