Mar 17, 2011

MTANZANIA AFANYISHWA KAZI KAMA MTUMWA UINGEREZA

Mmama wa miaka 47 aitwae Mwanahamisi Mruke,ni mwanamke alieajiriwa na mwanamke seeda khan kwa kumfanyia kazi za nyumbani huko uingereza.mwanahamisi alichukuliwa na huyo mama mwaka 2006 toka Dar na
kumpeleka uk katika mji wa Harrow north west london.Kwa makubaliano ya kwamba atamlipa pound 50kwa mwezi ambayo ni sawa na 120,000sh za kitanzania ambayo atakuwa anaituma direct kwa mwanae anaesoma chuo ili alipie ada.
                    House belonging to Saeeda Khan, 68, of Whitmore Road, Harrow,   nyumba aliyokuwa anafanyia kazi mama wa tz

ila huyo bosi wake alibadilika kazi haikwenda kama walivyoelewana akawa anafanyishwa kazi masaa 20 kwa siku bila mapumziko,bila malipo na alimnyang'anya passport yake ili asimkimbie huyo mwajiri wake.Mwanahamisi alikuwa akishindia slace za mikate miwili siku nzima na akinyimwa chakula na huyo mwajiri wake.
                                       Saeeda Khan
                         SEEDA KHAN MWAJIRI WA MWANAHAMISI.
 
Mwanahamisi alikuwa akilala jikoni, ndani ya miaka mitatu na huyu mama aliweka kengele alalapo mwanahamisi akipiga tu anamka na kwenda kumuudumia,mwanahamisi wazazi wake walifariki alikataliwa na mwajiri wake kwenda tanzania kwenye mazishi na binti yake aliolewa bila yeye kuudhuria.
Mwanahamisi  alibahatika kumriport mwajiri wake na alifunguliwa kesi na mwanahamisi ameshinda ,mwajiri wake atamlipa pound 25,000 na atafungwa miezi 9 nakupigwa faini ya pound 15000 kwa selikali.
 
                             
                            MWANAHAMISI MRUKE

                 

1 comment:

Anonymous said...

HURUMA JAMANI WA2 WENGINE WANA ROHO MBAYA KWELI KAZI AFANYE NA CHAKULA UMNYIMEE.MUNGU ATUHURUMIE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...