Jul 13, 2011

SPANX HUSAIDIA KUPUNGUZA MINYAMA UZEMBE NA KUKUPA SHAPE NZURI

Wanawake wengi wamekuwa na tatizo la kutokuwa comfortable na miili yao baada ya kunenepa au kuzaa na mwili umejiachia ukakatika na kuwa na minyama uzembe ,kama tumboni na sehemu za kiunoni.
hizi ndio spanx zenyewe kunandefu na fupi

Spanx ni nguo ya ndani ambayo inabana hizo extra nyama ulizozipata kiunoni au tumboni zikabana na kuonekana nashape nzuri ,mimi binafsi nilikuwa nazitumia baada ya kujifungua mwanangu nilikuwa na kile kitambi cha uzazi na ilinisaidia na hata likapunguka hii ni nzuri kuzidi kufunga kangha kwa wale waliotoka jifungua haina usumbufu kama kangha inakuwa imefunga ukaze tena. .

ila kunatatizo moja la hizi spanx kama unajijua unakitambi kikubwa alafu ukawa umeivaa hii spanx jaribu kuvaa nguo ambayo haita kubana sana ,ikikubana utaonekana vibaya mno


Jenny hudson alipokuwa mnene alikuwa mpenzi wa spanx ila hapa akavalia nguo ya mpira wakati anakitambi kikubwa matokeo yalikuwa hivyo.


na kunawale wengine hawana minyama uzembe ila nyuma hawana matako mazuri ya kuvaa nguo ya kubana na wanapenda wavae nao hao wanaweza zivaa.

Macelebrity wengi wanavaa spanx hasa wakiwa kwenye red carpet utaona mtu hana kitambi kumbe kakibana kwa ndani.
beyonce nae yumo kwenye spanx ,shost usijifadhaishe kanunue na wewe uvae ujihisi comfortable na mwili wako na ukavaa chochote unachojisikia kwa wale walio sweden Åhlens zipo kr 400 na kuendelea walioafrica nadhani shamimu anazo dukani kwake na wengine mnaweza kununua online kila lakheri wapenzi.

1 comment:

Anonymous said...

asante jalux mana umenisaidia mno

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...